Resumo do episódio
Hii leo tunaangazia mauaji yanayotokana na migogoro ya kimahusiano, tukichunguza takwimu zilizopo, na sababu zinazochangia ukatili huo.
Hii leo tunaangazia mauaji yanayotokana na migogoro ya kimahusiano, tukichunguza takwimu zilizopo, na sababu zinazochangia ukatili huo.
Episódios
Mauaji katika ndoa na migogoro ya kimahusiano Afrika Mashariki
OuvidoHii leo tunaangazia mauaji yanayotokana na migogoro ya kimahusiano, tukichunguza takwimu zilizopo, na sababu zinazochangia ukatili huo.
Teknolojia ya anga na matumaini mapya kwa jamii za bonde la Ziwa Victoria
OuvidoKatika mwambao wa Ziwa Victoria, mamilioni ya wananchi wanategemea kilimo, uvuvi na ufugaji wa samaki kwa ajili ya chakula na kipato. Hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi, kutotabirika kwa hali ya hewa na changamoto za uzalishaji vinaendelea kuathiri maisha yao. Je, teknolojia za satelaiti zinaweza kumsaidia mkulima kujua wakati unaofaa kupanda, mvuvi kufanya maamuzi sahihi na mfugaji wa samaki kupunguza hasara? Kupitia mradi wa KijaniSpace unaotekelezwa Tanzania, Kenya na Uganda kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya, teknolojia za anga na taarifa za kidijitali zinatazamwa kama sehemu ya suluhisho la changamoto hizo. Karibu katika Makala ya Afrika Mashariki, hii leo tunaangazia namna ubunifu wa kiteknolojia unavyoweza kubadili maisha ya wananchi wanaoishi katika bonde la Ziwa Victoria.
Urembo kwa njia ya upasuaji
OuvidoKaribu katika makala ya Afrika mashariki inayochunguza uhusiano kati ya urembo, kujiamini na shinikizo la kijamii. Tutaangazia simulizi za mwanawake aliyechagua kufanyiwa upasuaji wa urembo, pamoja na mitazamo ya wataalamu na wananchi.
Afrika Mashariki: Nishati Safi na Mustakabali wa Afrika Mashariki
OuvidoWiki hii tumeangazia namna nishati safi na umeme wa uhakika inavyoibadilisha Afrika. Afrika Mashariki imeendelea kushuhudia ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta ya nishati. Tanzania imeongeza uwezo wake wa uzalishaji wa umeme kufikia takribani megawati 4,600 baada ya kuanza kwa uzalishaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere wenye uwezo wa MW 2,115. Kwa upande mwingine Ethiopia imeendelea kuongoza ukanda kupitia mradi wa GERD wenye uwezo wa MW 5,150, huku Kenya ikiendelea kuwa kinara wa nishati ya jotoardhi na Uganda ikiendelea kuimarisha uzalishaji kupitia miradi mikubwa ya umeme wa maji.
Kenya: Nafasi ya vijana kwenye siasa za Kenya kuelekea uchaguzi mkuu 2027
OuvidoTunaangazia siasa za Kenya na nafasi ya vijana katika hatua za awali za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Je, vijana wanaingia kwenye uwanja wa siasa kama wapiga kura tu, au wanataka kuwa wabeba jahazi la maamuzi ya taifa?